Tafurwa: ZATU si chama cha siasa badala yake ni chama cha kutetea maslahi ya walimu nchni - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, March 10, 2018

Tafurwa: ZATU si chama cha siasa badala yake ni chama cha kutetea maslahi ya walimu nchni

HABARI KUUzatu
Akizungumza na Zanzibar24  Wakati wa Mafunzo ya kuwajengea  uwezo wa utendaji viongozi wapya waliochaguliwa kwa ajili ya  kuwaongoza wanachama katika chama hicho Katibu Mkuu wa chama cha walimu Mussa Omar Tafurwa amesema lengo kuu la kuanzishwa chama hicho  ni kutetea maslahi ya walimu nchni lakini wapo baadhi yao hukishirikisha  chama hicho  katika misingi ya kisiasa jambo ambalo ni kosa kisheria kwani chama hicho hakipo kisiasa kama baadhi yao wanavyodhani.
Amesema  ili kwenda sawa na sheria pamoja na kanuni  zilizopo chama  hakita kumvulia mwanachama yoyote atakae bainika kuvunja maadili ya chama hicho kwa kujiingiza katika siasa, ambapo amesema  kwa hatua za awali atakapo bainika  kiongozi atasimamishwa uongozi  au kuachishwa kazi moja kwa moja.
Kwaupande wao baadhi ya Viongozi Waliopatiwa mafunzo hayo ya uongozi wameahidi  kufanya kazi kwa mujibu wa sheria pamoja na kufuata miko na maadili ya chama ili lengo la chama hicho liweze kutimia na kutoa wito kwa wezao  kuzidisha bidii  katika kutoa taalum na kuwachana na itikadi za kisiasa ambazo zinaweza kukatisha njiani ndoto cha chama hizo.
Chama cha walimu zatu kimeandaa mafunzo hayo ya siku tatu  kwa walimu ambao ni viongozi  wapya waliochaguliwa ili kutetea maslahi ya walimu  wa Zanzibar.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI