Tetesi za
Soka Ulaya Jumatatu 26.11.2018: Dembele, Gomes, Hazard, Fabregas, Rice, Alba

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27 amekana kuwa atahamia
Paris St-Germain, lakini amekiri kuwa ataondoka Stamford Bridge msimu huu.
(Canal+ via Goal)
§
Mkurugenzi wa Milan Leonardo ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo
na Chelsea kuhusu kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31, na walinzi Gary Cahill, 32,
na Andreas Christensen, 22. (Football Italia)
Manchester
United ilituma maajenti kumtazama kijana mlinzi wa West Ham Declan Rice, 19,
wakati Hammers walishindwa kwa mabao 4-0 na Manchester City siku ya Jumamosi.
(Metro)
Beki wa Barcelona Jordi Alba, 29, amekiri kuwa hajapewa mkataba
mpya klabuni na kuacha hatma yake gizani. (ESPN)
Manchester
United wanaweza kungoja kumsaini kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini
baada ya kugundua kuwa kupengee cha kuuvunja mkataba wake kinaweza kutumiwa
mwisho wa msimu. (Mirror via Manchester Evening News)
Mlinzi wa
Chelsea David Luiz alifichua kuwa Maurizio Sarri amekuwa mwenye hasira zaidi
wakati wa ushindi kuliko wakati wa kushindwa kwao na Tottenham. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Everton Seamus Coleman, 30, ametaja rekodi yake
dhidi ya Liverpool kama ya kutia aibu. (Express)
Mshambulizi wa Santos Gabriel Barbosa, 22, anaweza kuwa tayari
kwa jukumu moja huko Toffees baada ya kipindi kigumu huko Inter Milan. (Tutto
Mercato Web - in Italian)
Mlinzi raia
wa Sweden Mikae Lustig, 31, anatarajiwa kufanya mazungumzo wiki mbili
zinazokuja ikiwa ataamua kuendelea kuwepo huko Celtic. (Daily Record)
Nahodha wa Leicester Wes Morgan, 34, ameitisha mazungumzo na
marefa kuhusu maamuzi yasiyo ya kuridhisha. (Leicester Mercury)
Kipa wa
Manchester United David de Gea atajiunga na Paris St-Germain msimu ujao wakati
mkataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Uhispania utakamilika huko Old
Trafford. (Mail on Sunday)
Inter Milan wanaweza kumpa meneja Jose Mourinho wachezaji ambao
amekuwa akiwatafuta kwa muda mrefu - mlinzi raia wa Slovekia Milan Skriniar,
23, na wing'a raia wa Croatia Ivan Perisic kama sehemu ya makubaliano. (Sunday
Mirror)
Meneja wa Newcatsle Rafael Benitez anatafutwa na klabu ya China
ya Guangzhou Evergrande. Mhispania huyo yuko mwaka wake wa mwisho huko St
James's Park. (Sun on Sunday)
Kipa wa
Columbus Crew na Marekani, Zack Steffen, 23, ataletwa na Manchester City kama
kipa wa ziada wa raia wa Brazil Ederson, 25. (Sun on Sunday)
Guardiola anasema kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 33,
atapumzishwa wakati wa shughuli nyingi za City za msimu huu. (Manchester
Evening News)