Rais JPM: Kuna watu hawapendi kuona amani hii tuliyonayo - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, March 10, 2018

Rais JPM: Kuna watu hawapendi kuona amani hii tuliyonayo

HABARI KUUmagufuli

Rais JPM: Kuna watu hawapendi kuona amani hii tuliyonayo


Rais John pombe Magufuli amesema ushuru ni ugonjwa ambao umeendelea kuwa kero kwa wafanyabiashara ndogondogo nchini.
“Ushuru ni ugonjwa , kila sehemu ushuru, ushuru , wabunge wenu wameshapitisha sheria. Mtu akiwa na chini ya tani moja ya mzigo asitozwe ushuru. Kwenye minada kulikuwa hata na ushuru wa kwato za ng’ombe, hivi unaweza kulizuia ling’ombe lisiwe na kwato?, “ amehoji Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 10, 2018 wakati akizindua barabara ya kilometa 45 kutoka Uyovu hadi Bwanga wilayani Bukombe, mkoani Geita iliyojengwa kwa kiwango cha lami ujenzi amabao umetumia asilimia 100 ya fedha ya ndani hadikukamilika.
Huku akizungumza mara kwa mara Kisukuma na kuwafanya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wa barabara kuangua kicheko, Magufuli pia alikemea kundi la watu aliodai kuwa hawapendezwi na kasi ya mafanikio katika sekta mbalimbali.
“Kuna watu hawapendi kuona amani hii tuliyonayo. Dhana halisi ya kutunza amani, amani ni kitu muhimu, hata mitume walihubiri amani, Yesu aliwaambia nawaachieni amani, kwa hiyo nawaambia amani tuliyonayo imejengwa na Mwalimu (Julius Nyerere), amekuja Mwinyi (Ali Hassan) na akaja KIkwete (Jakaya) pia ameitunza amani,” amesema.
“Tuwazuie dhahabu, tutengeneze reli kutoka Dar ,Dodoma, mpaka Lusumo na iwe ya umeme, nani anafurahi? Nani hafurahi kuona barabara za lami zikijengwa?.”
Chanzo: Mwananchi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI