WAKATI SIMBA WAKISUBIRI MABAO KIBAO TAIFA JUMAPILI, TEGETE ATAMBA KUWATIBULIA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, January 27, 2018

WAKATI SIMBA WAKISUBIRI MABAO KIBAO TAIFA JUMAPILI, TEGETE ATAMBA KUWATIBULIA

HABARI KUU




Mkuu wa Simba Mfaransa, Pierre Lechantre anatarajiwa kukaa kwa mara kwanza kwenye benchi la timu hiyo kesho Jumapili wakati watakapoivaa Majimaji ya Ruvuma, lakini amechimbwa mkwara na straika wa wapinzani wao hao.

Jerry Tegete ambaye ni straika wa Majimaji FC inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, amedai anataka kuvuruga ‘fungate’ la Simba na kocha huyo ambaye ameanza kazi Jumanne wiki hii.

Majimaji itaivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo awali Majimaji ilitoka sare ya bao 1-1 na Yanga mkoani Ruvuma.

Kocha wa Simba alitua nchini wiki iliyopita na kusaini mkataba wa miezi sita wa kuifundisha timu hiyo akiwa pamoja na msaidizi wake raia wa Tunisia, Mohammed Aimen.

Tegete alisema ujio wa kocha huyo mpya hauwafanyi wao waogope na kupata matokeo mabaya, kwani wataingia uwanjani kwa ajili ya ushindi pekee.

“Kama unavyojua ligi inaelekea katika mzunguko wa pili, hivyo ni lazima tushinde michezo yote iliyokuwepo mbele yetu ili tujiweke katika nafasi nzuri katika msimamo,” alisema Tegete.

Alisema walianza na sare mbili kutoka kwa timu kubwa zenye upinzani mkubwa ambazo ni Azam FC na baadaye Singida United, hivyo wanaofuata ni Simba.


 “Tunajua Simba wameleta kocha mpya Mfaransa, lakini hiyo haitufanyi sisi kuwaogopa, kwani tuna timu imara itakayoleta ushindani, tumetoka sare na Azam na Singida United ambazo pia zina makocha Wazungu, hivyo tunakwenda kucheza na Simba tukifuata matokeo mazuri ya ushindi na siyo kitu kingine,” alitamba Tegete.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI