NYOTA SERENGETI AFUZU SOKA LA KULIPWA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, November 03, 2018

NYOTA SERENGETI AFUZU SOKA LA KULIPWA

HABARI KUU

Nahodha wa Serengeti Boys, Morice Abraham amefanikiwa kufuzu majaribio yake ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya vijana (U17) ya Midtylland ya Dernmak.

Morice alirejea nchini hivi karibuni akitokea Denmark ambako alikuwa huko kwa majaribio ya wiki mbili na sasa yupo kwenye kambi ya Serengeti inayojiandaa na michuano ya COSAFA itakayofanyika Botswana Desemba, mwaka huu.

Wakati Morice akitusua, Mtanzania mwingine Kelvin John ‘Mbappe’, naye amegeuka kivutio kwa walimu wa timu ya HB Koge ya Denmark ambako anafanya majaribio kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka.

Morice amelimbia Championi Jumamosi kuwa, baada ya kurudi nyumbani alipokea taarifa kwa mdomo kuwa amefanikiwa kufuzu majaribio yake na tayari barua ya uthibitisho imemfikia hivyo muda wowote ataelekea Denmark baada ya kukamilisha mipango yake.

“Barua ya majibu imeshakuja na sasa uongozi wangu ukiongozwa na kocha Oscar Mirambo (Kocha wa Serengeti Boys) unafanya utaratibu wa kuangalia nitakwenda kuishi katika mazingira gani, hasa katika suala la elimu kwa kuwa bado sijamaliza masomo hivyo mwalimu anahitaji kufahamu nitasomaje nikiwa kule,” alifunguka Morice.

Kwa upande wa meneja wa Kelvin ambaye yupo naye Denmark, Mbaki Mutahaba amesema mchezaji wake anaendelea vizuri huku walimu wa kituo alichopo wakionyesha kuvutiwa naye kutokana na kufanya kila anachoagizwa na walimu wake.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI