Afghanistan: Kituo cha mafunzo ya jeshi chavamiwa Kabul - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, January 29, 2018

Afghanistan: Kituo cha mafunzo ya jeshi chavamiwa Kabul

HABARI KUU
 Maafisa wa usalama wamefunga barabara za kuelekea eneo la shambulio
Milio ya risasi na milipuko imesikika katika kituo cha mafunzo ya kijeshi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, taarifa zinasema.

Vyombo vya habari vinasema Chuo Kikuu cha Masuala ya Ulinzi wa Taifa cha Marshal Fahim kimeshambuliwa mapema asubuhi.

Shambulio hilo limetokea baada ya shambulio lililowaua watu wengi zaidi miaka ya karibuni kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100 Jumamosi.

Shambulio hilo la Jumamosi lilitekelezwa kwa kutumia gari la kubebea wagonjwa lililokuwa limejazwa vilipuzi.

Wapiganaji wa Islamic State na Taliban wamekuwa wakitekeleza mashambulio maeneo mbalimbali nchini humo.

Shambulio hilo la Jumamosi lilitekelezwa wiki moja baada ya shambulio jingine katika hoteli moja ya Kabul kuwaua watu 22 - wengi wao raia wa nchi za nje.

Taliban walisema ndio waliotekeleza mashambulio yote mawili.

Taasisi za kijeshi zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo.

Oktoba 2017, makurutu 15 wa jeshi waliuawa kwenye mlipuko uliotokea nje ya kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Marshal Fahim, ambacho hupatikana magharibi mwa Kabul.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI