MAFARAO AL MASRY WAANGUKIA PUA KWA KIPIGO ZAMBIA, LAKINI NDIYO WANAOKUTANA NA SIMBA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, February 20, 2018

MAFARAO AL MASRY WAANGUKIA PUA KWA KIPIGO ZAMBIA, LAKINI NDIYO WANAOKUTANA NA SIMBA

HABARI KUU



Mafarao wa Misri, Al Masry wameangukia pua baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Hata hivyo, Al Masry wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya ushindi wao wa mabao 4-0 wakiwa nyumbani Misri na sasa hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho, wanakutana na Simba.

Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendamarie na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa idadi ya mabao 5-0.

Maana yake, Simba inakwenda kukutana na mlima mwingine raundi ya mapema tu baada ya kurejea katika michuano ya kimataifa.

Mechi ya kwanza itaanzia jijini Dar es Salaam, kabla ya Simba kufunga safari na kwenda Misri kumalizia ngwe hiyo inayotarajia kuwa ngumu.


Simba ina heshima kubwa kwa kuwa imewahi kuivua ubingwa na kuing’oa mashindano Zamalek ya Misri, timu kubwa ya pili na moja ya klabu maarufu barani Afrika.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI