Pierre-Emerick Aubameyang: Arsenal wakaribia kumchukua mshambuliaji wa Borussia Dortmund kwa £60m - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, January 29, 2018

Pierre-Emerick Aubameyang: Arsenal wakaribia kumchukua mshambuliaji wa Borussia Dortmund kwa £60m

HABARI KUU
 Pierre-Emerick Aubameyang
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji matata kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kwa karibu £60m.

Lakini uhamisho huo hautaidhinishwa hadi pale Dortmund watakapopata mchezaji wa kujaza pengo ambalo litaachwa na Aubameyang.

Taarifa zinasema mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ni miongoni mwa wachezajia ambao wanatafutwa na klabu hiyo ya Ujerumani.

Gunners tayari walikuwa wamewasilisha maombi ya kutaka kumchukua Aubameyang mara mbili lakini yakakataliwa na Dortmund.

Aubameyang, 28, alianza kwenye mechi Dortmund kwa mara ya kwanza tangu 16 Desemba mnamo Jumamosi katika mechi ambayo walitoka sare na Freiburg.

Dortmund wamesema wako tayari kumuuza mchezaji huyo lakini iwapo "matakwa fulani yatatimizwa kikamilifu".

Klabu hiyo ya Bundesliga ilikataa ofa ya euro 50m (£43.64m) kutoka kwa Arsenal Jumatano.

Aubameyang alikuwa anatumikia anatumikia adhabu na hakuruhusiwa kucheza mechi yao dhidi ya Wolfsburg wiki mbili zilizopita baada yake kukosa kuhudhuria mkutano wa timu hiyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI