Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 19.04.2018 - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, April 19, 2018

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 19.04.2018

HABARI KUUKocha wa klabu ya New York City patrick Vierra miongoni mwa watakaomrithi WengerKocha wa klabu ya New York City patrick Vierra miongoni mwa watakaomrithi Wenger

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na mkufunzi wa klabu ya New York City nchini Marekani Patrick Vieira ni miongoni mwa wakufunzi walioorodheshwa kumrithi mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger atakapostaafu. (Mail)
Klabu ya Tottenham inataka kumnunua winga wa klabu ya Leicester 21 Demarai Gray. Tottenham ilitaka kumsajili Gray msimu wa dirisha la uhamisho ulioisha lakini The Foxes walikataa maombi yanayowasilishwa ya nahodha huyo wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 21 nchini Uingereza (ESPN)Mkufunzi wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anamtaka beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa, 25Mkufunzi wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anamtaka beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa, 25
Mkufunzi wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino anamtaka beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa, 25, lakini anaweza kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Chelsea kumpata raia huyo wa Ufaransa. (Mirror)
Lyon na Juventus wanataka kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22. (Sun)Anthony Martial
Anthony Martial

Arsenal pia walikuwa wanamnyatia lakini Wenger ameamua kuimarisha safu nyengine za kikosi chake mwisho wa msimu huu. (Evening Standard)
Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri ndio chaguo la kwanza la Chelsea kuchukua mahala pake Antonio Conte.
Wachezaji kadhaa wanaolengwa na Chelsea mwisho wa msimu huu hawataandikisha mikataba hadi watakapobaini ni nani atakayekuwa mkufunzi wa klabu hiyo. (Mail)
Mmiliki wa Chelsea Roman AbrahamovicMmiliki wa Chelsea Roman Abrahamovic

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ametakiwa kumsajili kinda anayeinukia badala ya wachezaji maarufu.. (Telegraph)
Hatahivyo usimamizi wa klabu hiyo unatofautiana kuhusu ni nani atakayemrithi raia huyo wa Ufaransa huku kocha wa zamani wa Barcelona Louis Enrique pia akilengwa. (Telegraph)
Liverpool inataka kumsaini kiungo wa kati wa Portugal Ruben Neves, 21, kutoka klabu mpya iliopandishwa daraja Wolverhampton Wanderers. (Talksport)LamelaLamela
Crystal Palace itamuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 27, mwisho wa msimu huu. (Mail)
Klabu ya Wolves iko tayari kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere, 26, ambaye huenda akaondoka Arsenal kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu na tayari klabu ya Everton imewasilisha ombi kubwa. (mirror)
Tottenham itaongeza kandarasi ya mshambuliaji Erik Lamela kwa mwaka mmoja hatua itakayomuweka mchezaji huyo wa Argentina katika klabu hiyo hadi 2020. (Independent)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI