Wanafunzi shuhulikieni yanayowahusuWanafunzi shuhulikieni yanayowahusu - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, April 19, 2018

Wanafunzi shuhulikieni yanayowahusuWanafunzi shuhulikieni yanayowahusu

HABARI KUU

Imeandikwa na  Khadija Mahmoud  , Pemba
WANAFUNZI wa kidato cha sita wa skuli yamchangamdogo wametakiwa kushughulikia masomo yao  badala ya kujihusisha na vishawishi vibaya vinavyopelekea kutofanya vizuri katika mitihani yao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Utumishi Wilaya ya Wete Faki Hamad Faki wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo huko katika Skuli ya Sekondar Mchanga Mdogo katika Maafali ya tano ya kuwaaga wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza masomo yao ya kidato cha sita hivi karibuni.
Amesema Vijana ndio nguvu kazi inayotegemewa na Taifa hivyo ni vyema kutumia muda wao vizuri katika kujitafutia elimu huku wakijiepusha na vikundi viovu.
Aidha  amesema watakapojiingiza katika mambo ambayo sio mazuri kwao watashindwa kufanya vizuri  katika mitihani yao ya kumalizia masomo.
Mapema mwalim Mkuu wa skuli hiyo Juma Said Hamad amesema Skuli hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa vikaliwa pamoja na walimu wa kufundisha masomo ya sanyansi hivyo kupelekea wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika masomo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi Juma Sleiman Juma amewataka wazazi kushirikiana na kamati ya skuli pamoja na walimu ili kuhakikisha wanawasimamia vyema wanafunzi katika masomo yao na kuwashauri vijana wale ambao hawatafaulu katika mitihani yao  wajiendeleze katika vyuo vya amali ili waweze kupata ujuzi kupitia vyuo hivyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI