PIGO ARSENAL, LACAZETTE NJE WIKI SITA BAADA YA UPASUAJI - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, February 14, 2018

PIGO ARSENAL, LACAZETTE NJE WIKI SITA BAADA YA UPASUAJI

HABARI KUU

TIMU ya Arsenal inaweza kumkosa mshambuliaji wake, Alexandre Lacazette kwa wiki sita baada ya Mfaransa huyo kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kushoto.
Klabu imethibitisha Lacazette aliumia goti na kufanyiwa upasuaji jana asubuhi na atakuwa nje kwa wiki sita baada ya zoezi hilo.
Arsenal imesema upasuaji wa goti hilo umetokana na tatizo dogo, lakini Lacazette atapatiwa tiba zaidi. 
Lacazette alipoteza nafasi mbili nzuri za kusawazisha Jumamosi Arsenal ikifungwa 1-0 na mahasimu wao wa London, Tottenham baada ya kuingia akitokea benchi. 
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexandre Lacazette atakuwa nje kwa wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji PICHA ZAIDI SOMA HAPA 
Mfaransa huyo alijiunga na klabu kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 52, lakini rekodi yake ilivunjwal na Pierre-Emerick Aubameyang aliyewasili Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 56.
Lacazette alitarajiwa kuingoza safu ya ushambuliani ya Arsenal katika mechi ya Europa League dhidi ya wenyeji, Ostersunds FK, lakini maumivu yanamuondoa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Lyon atakosekana pia kwenye fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City Uwanja wa Wembley on February 25.
Lacazette alikuwa ana mwanzo mzuri Emirates akifunga mabao manne katika mechi sita za kwanza tangu asajiliwe kuroka Ufaransa, lakini tangu hapo amefunga bao moja tu kati ya 13.   

MECHI AMBAZO ARSENAL ZITAMKOSA ALEXANDRE LACAZETTE 

 Februari 15 – Ostersunds (away) – Europa League last-32
Februari 22 – Ostersunds (home) – Europa League last-32
Februari 25 – Man City (Wembley) – Carabao Cup final
Machi 1 – Man City (home)
Machi 4 – Brighton (away)
Machi 11 – Watford (home)
Machi 17 – Leicester (away) 

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI