Manula uhakika golini kuwazuia Gendarmerie - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, February 20, 2018

Manula uhakika golini kuwazuia Gendarmerie

HABARI KUU
Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amethibitisha kwamba golikipa namba moja wa klabu hiyo Aishi Manula atacheza mchezo wa marudiano wa Caf Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti.

Jana jioni zilienea picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Manula akiwa amefungwa bandage mkononi baada ya kuumia mkono wa kushoto na ikaelezwa huenda akaukosa mchezo wa leo kutokana na maumivu hayo. Masoud amesema John Bocco peke yake ndiyo hayuko fit kwa ajili ya mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa VPL dhidi ya Mwadui.

“Aishi yuko vizuri watanzania wote wajue, kweli jana alipata tatizo mazoeni lakini yuko vizuri na atacheza mechi, wapenzi wa Simba waache wasiwasi wazidi kutuombea tufanye vizuri.”

“Wachezaji wote wako tayari isipokuwa nahodha John Bocco ndiyo atakosekana lakini wengine wote watakuwepo kwa ajili ya kupambana kwa ajili ya mechi ya leo. Tunajua sio kazi rahisi lakini tutapambana kama kawaida yetu mwanzo wa mechi hadi mwisho tuhakikishe Simba inasonga mbele.”

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI