ZECO yajipanga kuboresha huduma ya nishati ya umeme - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, January 28, 2018

ZECO yajipanga kuboresha huduma ya nishati ya umeme

HABARI KUU
 
Shirika la Umeme Zanzibar ZECO limekusudia kuimarisha  huduma ya Nishati ya Umeme kwa wananchi ili kuwaondoshea usumbufu wanaokumbana nao wakati wakihitaji huduma hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baaada ya Kufunga mafunzo ya Siku tatu kwa taasisi Zinazosimamia Nishati Zanzibar, Meneja Mkuu wa Shirika hilo Hassan Ali Mbarouk amesema kutokana na mafunzo waliopewa wasisimamizi wa taasisi za Nishati ,wataweza kutoa huduma Bora kwa wananchi.

Amesema katika mafunzo hayo wamejifunza namna Bora ya Ununuzi na Njia sahihi ya kuuunganisha Mitandao ya Shirika hilo kwa Mfumo maalum kupitia Mita za tukuza katika kipindi cha miaka miwili ijayo .

Pia watawewezesha watowa huduma na kujua namna ya kuwahudumia wateja wao ili waweze kuzuia mapato ya serikali yasipoteee katika manunuzi .

Kwa upande wake Afisa Mdhamini wa Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Pemba Juma Bakari Alawi amesema ili mafunzo hayo yaweze kufikia malengo waliyokusudiwa ni vyema kwa wananchi kuendelea kulipia huduma hiyo bila kushurutishwa ili kuliwezesha Shirika la ZECO kuweza kutoa huduma ya Nishati kwa wananchi.

Amesema ZECO ni shirika linalojitegemea katika kutoa huduma kwa wananchi hivyo wananchi kutolipia huduma hiyo na wakati na kwa kufuata sheria kusababisha  kuzorota kwa huduma hiyo.

Semina hiyo ya Siku tatu iliyofanyika kilimani Mjini Zanzibar imeshirikisha wadau mbali mbali wa shirika hilo Wakiwemo Viongozi wa Bodi ya ZECO pamoja na watendaji wa Wizara ya Ardhi ,Maji ,nishati na Mazingira ikiwa na lengo la kujifunza namna ya kuimarisha utoaji wa huduma ya Nishati kwa Wananchi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI