RIDHIWANI KIKWETE AHUSISHWA KUCHUKUA NAFASI YA MANJI YANGA, ATOA TAMKO HILI - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, May 09, 2018

RIDHIWANI KIKWETE AHUSISHWA KUCHUKUA NAFASI YA MANJI YANGA, ATOA TAMKO HILI

HABARI KUU

Shabiki wa Yanga, Ridhiwani Kikwete, amehusishwa kugombea nafasi ya uongozi wa Uenyekiti ndani ya klabu hiyo ambao umeagizwa kufanyika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Baada ya taarifa hizo kuenea, Ridhiwani amesema kuwa yeye hana mpango wa kuchukua nafasi hiyo kutokana na majukumu mengine ya kiserikali yanayomkabili.

Akizungumza na radio EFM asubuhi hii, Ridhiwani ameeleza kuwa yeye si Mwanachama wa Yanga hivyo anakosa kigezo hicho cha kuwania nafasi hiyo ya juu katika uongozi ndani ya klabu hiyo.

Mbali na majukumu ya kiserikali, Ridhiwani ameeleza pia kuwa aliwahi kusemwa na mmoja wa kiongozi wa Yanga miaka kadhaa nyuma akielezwa kuwa hana mamlaka ya kuzungumza chochote kuhusiana na klabu hiyo.

Kitendo cha kuambiwa kuwa hana mamlaka ya kuongea chochote, huku akitajwa kuwa hajalipia kadi ya uanachama ndani ya Yanga, kinamfanya asipate nguvu ya kugombea nafasi hiyo.

Kiongozi huyo amesema ni wanachama na mashabiki ndiyo wamekuwa wakipendekeza agombee na si yeye kuwa amehitaji kufanya hivyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI