George HW Bush: Mbwa wa rais wa zamani Sully agusa wengi kwa heshima zake za mwisho - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


nuru+ya+habar

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Thursday, December 06, 2018

demo-image

George HW Bush: Mbwa wa rais wa zamani Sully agusa wengi kwa heshima zake za mwisho

Responsive Ads Here

_104603418_p06tnb58
Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSully akiwa katika chumba ulimokuwa mwili wa marehemu George HW Bush katika makao makuu ya Bunge la Marekani

Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa rais wa zamani wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.
Bw Bush, aliyehudumu kama rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989 na 1993 alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa na miaka 94.
Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, alisafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas kwenda Washington DC siku ya Jumatatu.
Jeneza lenye mwili wake lilisafirishwa kwa ndege kutoka Texas kwenda DC kwa ndege ya Air Force One - ambayo kwa muda ilipewa jina Special Air Mission 41, kwa heshima ya rais huyo.
Mwili huo ulirejeshwa Texas Jumatano.


_104593032_d19d886f-9236-45f9-bfff-ff3b11034526Haki miliki ya pichaOFFICE OF GEORGE HW BUSH
Image captionPicha ya kwanza ya Mbwa Sully akiwa amelala karibu na jeneza lenye mwili wa George HW Bush iliyowagusa wengi

Mbwa huyo wa jina Sully alisindikiza jeneza hilo muda wote.
Picha ya kwanza kabisa ya Sully akitoa heshima zake ilipakiwa mtandaoni na msemaji wa Bw Bush Jim McGrath, pamoja na ujumbe: "Mission complete."


_104599981_050973533Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSully alisafiri na Air Force One iliyoubeba mwili wa marehemu kwenda Washington Jumatatu

Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao.


_104599983_050972906Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionAlirejea vivyo hivyo Texas Jumatano

Post Bottom Ad

HABARI

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *