UGANDA YAWEKA KINZINGITI KIZITO KWA STARS - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, November 20, 2018

UGANDA YAWEKA KINZINGITI KIZITO KWA STARS

HABARI KUU
Raisi wa nchi ya Uganda, Yoweri Museven amesema kuwa licha ya timu yake kufanikiwa kufuzu kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) wanapaswa kushinda mchezo wao wa mwisho.

Uganda wamefanikiwa kufuzu baada ya kufikisha pointi 13 katika kundi L ambalo wapo pamoja na Tanzania ambayo ilipoteza nafasi hiyo baada ya kufungwa na Lesotho.


"Natambua kwamba mmefanikiwa kufuzu kushiriki Afcon na natambua kuwa mmebakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Tanzania, tafadhali hakikisheni mnashinda msipoteze," alisema.


Tanzania imejiweka kwenye mtego katika kundi L ili  kuweza kupenya kwenye hatua hii ni kuhakikisha wanaifunga Uganda na kusubiri matokeo ya Cape Verde kumfunga Lesotho ama kutoa sare.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI