Kwamtipura kumeoza, Manispaa wakumbushwa kutekeleza majukumu yao - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, November 20, 2018

Kwamtipura kumeoza, Manispaa wakumbushwa kutekeleza majukumu yao

HABARI KUU

Tunafahamu kwamba Zanzibar  inahistoria kubwa juu ya ugonjwa wa kipindupindu  ambao husababishwa na uchafu wa mazingira, pamoja  na kutokuwa na uwangalizi  katika uhifadhi wa taka zetu.

Niukweli ulio wazi  kuwa  Serikali kwa kushirikiana na Mabaraza ya  Manispaa ya Zanzibar  wameweza  kupiga  hatua  katika harakati za kutunza mji  wa Zanzibar pamoja na vitongoji  vyake ikiwemo  kufanywa  usafi  katika maeneo  mbalimbali,  kuwekwa madebe na makontena  ya kuhifadhia taka  katika mitaa  mbalimbali na kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya kutunza mazingira na matumizi ya vyoo katika majumba yao.

Zipo  sehemu hapa Zanzibar  bado kuna baadhi ya  wananchi hawana utamaduni  wa kuyatumia makontena  katika kuhifadhia  taka  zao  na kuamua kwa makusudi  kumwaga takataka na uchafu sehemu yeyote wanapoamua na wapo wengine  wanayatumia vyema makontena na madebe ya kuhifadhia taka  hadi  kujaa na kuzimwagia chini  ya kontena.

Wananchi wa Kwamtipura Shehia ya Kivumbi  walia na hali ya uchafu pamoja na harufu mbaya za taka zilizohifadhiwa kwenye makontena katika maeneo yao ambazo  huchelewa kuja kuchukulia na Baraza LA Manispaa  ili kwenda kutupwa sehemu  husika  jambo linalowatia hofu usalama  wa afya zao.

Mwandishi  wa Zanzibar 24 ameshuhudia taka zilivyojaa katika kontena hadi kumwagika  chini na kutoa harufu mbaya huku watoto wakicheza karibu na kontena hilo lililokaribu na makaazi ya watu hali ambayo inatia  hofu ya kutokea kwa maradhi ya mripuko ikiwemo matumbo ya kuharisha na kipindupindu.

Ushauri  ni jambo  zuri, Tunawaomba Mamlaka husika  msisubiri  kuitwa  muwe  mnakagua makontena ya taka  Mara kwa Mara ili kuondoa  kero hizi za kila siku na baadae kuwabebesha lawama wananchi kwa madai hawakubaliani na jukumu la kusafisha mazingira yao.

Zipo baadhi  ya sehemu asubuhi na jioni  mnakwenda kuchukua taka hasa  katika maeneo  ya mjini mfano  darajani na maeneo  mengine  ya karibu  na mji  lakini maeneo  ya N’gambu mnajisahau hadi wiki  ndio mnapita  jambo ambalo  kiutendaji mnakosa ufanisi.

Amina Omar.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI