Serikali kuwapandisha cheo Askari walionusurika kifo wakipambana na Majambazi - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, November 25, 2018

Serikali kuwapandisha cheo Askari walionusurika kifo wakipambana na Majambazi

HABARI KUUMh. Kangi Lugola                                                                                                                                     
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola amemhakikishia Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Jonathani Shanna kuwa atawapandisha vyeo askari waliofanikisha kuua majambazi Novemba 16.
Akiongea  jijini Mwanza ambapo yupo kwenye ziara ya kikazi, Kangi amesema anatambua kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi mkoani humo huku akiweka bayana kuwa askari waliojeruhiwa kwenye mapambano na majambazi wameonesha ushujaa kwani ni kosa kwa askari kuwa mwoga.
“Kwenye sheria yetu ya Jeshi la polisi na polisi wasaidizi sura ya 322, ukienda kwenye makosa ya kinidhamu ya askari, ni kosa kwa askari kuwa mwoga,”askari hupaswi kukimbia tukio’ lazima ukabiliane nalo”, amesema.
”Nikuhakikishie Kamanda Shanna wale vijana wote waliofanya kazi kubwa kwenye tukio la juzi kukabiliana na majambazi, mimi kama Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kwa amri ya Serikali tutawapa zawadi ya kuwapandisha vyeo”,aliongeza Kangi Lugola.
Jumla ya watu saba wanaodaiwa kuwa majambazi waliuawa katika mapambano ya kujibizana kwa risasi na askari polisi katika tukio lililotokea alfajiri ya Novemba 16 katika eneo la mlima Kishiri jijini Mwanza.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI