Ndugai afunguka lengo la kutaja Mawaziri na Wabunge watoro - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, November 21, 2018

Ndugai afunguka lengo la kutaja Mawaziri na Wabunge watoro

HABARI KUUSpika wa Bunge, Job Ndugai                                                                                                         

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema lengo la kuwataja Mawaziri na Wabunge ambao wana mahudhurio hafifu ndani ya Bunge haikuwa kuwachongea kwa viongozi wa vyama vyao bali ni kuwataka wabunge hao kutimiza wajibu wao wa kuingia bungeni.


Kwa mujibu wa Spika Ndugai Mawaziri wengi wanashindwa kuhudhuria bungeni, kwa kisingizio cha  kuwa wako kwenye maeneo mbalimbali wanatatua changamoto za wananchi wakati wawakilishi wao wako bungeni.
Akizungumza na eatv Spika Ndugai amesema “nia haikuwa kumchongea mbunge yeyote, kumbuka hata mawaziri nao wanakuwa wabunge kabla ya kuwa mawaziri, na uzuri wa bunge letu linaratiba ya mwaka mzima, wanapokuja pale wanakuja na ratiba nchi nzima,
haiwezekani mimi mbunge wa Kongwa bunge linaendelea halafu Waziri anaenda Kongwa
.”
Kwa sasa siwezi kuwataja tena, orodha ya wabunge ambao ni watoro ila kwa faida ya wananchi tutawatajia mwishoni ili inapofika kipindi cha uchaguzi, watambue ni mbunge gani ambaye walimuagiza bungeni lakini alikuwa ahudhurii,” amesema.
Mfano huyo Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema,) kutwa yuko kwenye mitandao ya kijamii anadhani ubunge ni mtandaoni, na hata hao mawaziri niliwaambia wawajibu wapinzani kwenye mitandao ya kijamii sikumaanisha wasije bungeni wanatakiwa pia wafike bungeni,” ameongeza Ndugai
Wiki iliyopita wakati wa Mkutano 13 wa Bunge Spika Job Ndugai aliwataja orodha ya wabunge na Mawaziri ambao ni watoro bungeni akiwemo Waziri Januari Makamba, Palamagamba Kabudi, na kwa wabunge alimtaja Godbless Lema.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI