Fuoni watakiwa kutumia 113 kutoa taarifa za rushwa - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, November 21, 2018

Fuoni watakiwa kutumia 113 kutoa taarifa za rushwa

HABARI KUU
Wakaazi wa shehia ya Fuoni Migombani wamewaomba wananchi wenzao kuacha tabia ya kutoa na kupokea rushwa pale wanapofika katika taasisi za umma kwa ajili ya kupata huduma.
Wakizungumza kwa sheha wa shehia hiyo Ramadhan Mwadini Khatib, wamesema endapo wananchi wenyewe wanajidhatiti kuacha kutoa rushwa pale wanapofika katika taasisi za umma kwa ajili ya kupata huduma itasaidia kudhibiti vitendo hivyo.
Aidha wamesema ni vyema taasisi zinazotoa huduma kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi.
Hamad Khatib na Yahya Salum, walisema iwapo watendaji watafanya kazi kwa uadilifu bila kuuza haki za wananchi wanapotaka huduma, itasaidia kuondoa tatizo la rushwa.
“Maeneo ambayo kuna wimbi kubwa la watu kupokea rushwa ni maeneo ya huduma za kijamii ikiwemo hospitali, mahakamani na polisi, ZAECA waangalie sana kwani watu kila siku wanakamatwa na dawa za kulevya lakini hakuna hatua zinazochukuliwa,” walisema.
Walitumia fursa hiyo kuviomba vyombo vya ulinzi kuhakikisha vinaacha muhali na badala yake vitekeleze majukumu yao ipasavyo.
Sheha wa shehia ya hiyo, aliwasisitiza wananchi kutoogopa kuitumia namba ya ZAECA 113 pindi wanapoombwa rushwa ili kutoa taarifa na kudhibiti tatizo hilo.
Kaimu Mkurugenzi elimu kwa umma wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar, Sheha Kombo Hamad, alisema sheria zote zinasisitiza uadilifu katika kazi na sio kufanya kazi kwa kutegemea bahashishi kutoka kwa mteja.
Kikiao hicho kiliandaliwa na ZAECA ikiwa ni katika muendelezo wake wa kupita shehia mbalimbali kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na kupambana na rushwa.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI