Jeshi la Magereza lakanusha Lulu kuwa huru - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, November 13, 2018

Jeshi la Magereza lakanusha Lulu kuwa huru

HABARI KUU

Jeshi la Magereza limekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Mwanadada Elizabeth Michel maarufu Lulu ameshakuwa huru baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake cha nje.


Msemaji wa Jeshi la Magereza, Amina Kavirondo, amezungumzia sakata hilo na kutoa ufafanuzi juu ya kuachiwa huru kwa muigizaji huyo ambaye inasemekana amemaliza hukumu ya kifungo chake, akisema kwamba “Lulu bado ni mfungwa”
“Taratibu nafikiri zinaeleweka, anakuwa bado ni mfungwa, na anapokuwa na kifungo hicho cha nje kuna taratibu zake, akimaliza basi kuna taratibu kama mfungwa yeyote, hata kama ni maarufu. Kile ambacho Lulu atafanyiwa ndicho atakachofanyiwa mfungwa mwingine yeyote, ‘treatment’ yetu ni sawa na wafungwa wengine,” amesema.
Akizungumza na Eatv.tv Amina Kavirondo amesema kwamba utaratibu wa mfungwa yeyote anayemaliza kifungo chake lazima ufuatwe kwanza, ndipo aachiwe rasmi na Jeshi la Magereza, na ndipo anaweza kuwa huru na maisha yake.
“Kama hatukutangaza wakati wafungwa wengine wanatoka hata yeye hatutatangaza, na hakutakuwa na upendeleo, na mwenyewe anajua anatakiwa afanye nini, yule ni mfungwa kama wengine, hawezi kumaliza akaondokea kule kule”ameongeza Amina Kavirondo.
Muigizaji huyo anatarajiwa kumaliza kifungo chake mwezi huu, baada ya kubadilishiwa hukumu kutokana na msamaha wa Rais na kupewa kifungo cha nje, kwa kesi ya mauji bila kukusudia iliyokuwa ikimkabili hapo awali, ambapo alihukumiwa miaka miwili jela.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI