ALLIANCE KUZIFUMUA SIMBA NA YANGA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, November 13, 2018

ALLIANCE KUZIFUMUA SIMBA NA YANGA

HABARI KUU
Uongozi wa timu ya Alliance FC umefunguka kuwa kuelekea dirisha dogo la usajili watasajili wachezaji 8 wenye uzoefu kutoka timu kubwa kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye ligi kuu Tanzania Bara.

Ofisa habari  wa Alliance John Mwafulango amesema kuwa kikosi chake kina mapungufu makubwa kutokana na kutokuwa na wachezaji wenye uzoefu hivyo watafanya mipango ya kutumia dirisha dogo kufanya maboresho makubwa.

"Tutasajili wachezaji nane wenye uzoefu katika ligi kuu ikiwa ni pamoja na mlinda mlango, viungo, mabeki na washambuliaji ili kuendeleza makali yetu kwenye ligi, tutaangalia kwenye timu zote kubwa ikiwa ni pamoja na Simba, Yanga mpaka Azam kama mwalimu atawataka tutafanya usajili," alisema. 

Alliance wamecheza michezo 14 na kujikusanyoia ponti 13 ilikuwa ni timu ya kwanza kufungwa na Simba mabao 5-1, dirisha dogo la usajili litafunguliwa kesho.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI