- NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


nuru+ya+habar

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Thursday, August 30, 2018

demo-image
Responsive Ads Here
HABARI KUU
kuku
Mahakama ya wilaya Mkokotoni imemhukumu kutumikia chuo cha mafunzo mwaka mmoja kijana Haji Hamza Hija miaka 32 mkaazi wa Mkokotoni, mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kosa la wizi wa Kuku.

Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Nasour mbele ya hakimu Moh’d Thubeit kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 4, 2017 saa 4 usiku huko Mkokotoni ambapo alivunja nyumba na kuiba Kuku mmoja anayekisiwa kuwa na thamani ya Tsh, 20,000 mali ya Bi Mpaji Mtwana Fumu.

Kesi dhidi ya mshitakiwa ilifunguliwa mahakamani hapo Januari 2, 2018 na mashahidi watatu walitoa ushahidi wao lakini wakati wa kusikiliza ushahidi mtuhumiwa alitoroka mahakamani.

Akisoma hukumu Jana Agosti 29 hakimu Moh’d Thubeirt amesema mahakama imemkuta na kosa kijana Haji na inamuamuru kutumikia kifungo cha mwaka mmoja ili iwe fundisho kwake na vijana wengine wenye tabia kama yake.
Hukumu itaanza mara moja baada ya mshitakiwa kukamatwa.


Post Bottom Ad

HABARI

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *