Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara.
Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala ambaye amesafirishwa kwa ndege kutoka Arusha alikopata ajali leo asubuhi, kuja Jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Rais Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Dkt. Kigwangalla aliyekuwa akisafiri kutoka Arusha kwenda Dodoma amepata ajali leo majira ya saa 12:15 asubuhi katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kuumia.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Dkt. Kigwangalla amepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alipata ajali ya gari mkoani Manyara.
Katika mapokezi hayo Rais Magufuli alikuwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (aliyemsindikiza Dkt. Kigwangalla), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili Mej Jen. Gaudence Milanzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa kwa ajili ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza uwanjani hapo Rais Magufuli amempa pole Dkt. Kigwangalla na kumuombea apone haraka na pia amewashukuru madaktari na wauguzi wa Kituo cha afya cha Magugu walioanza kutoa huduma ya kwanza na amewashukuru Madaktari na wauguzi wa hospitali ya Selian iliyopo Mjini Arusha kwa juhudi kubwa walizofanya kuokoa maisha ya Dkt. Kigwangalla na majeruhi wengine wa ajali hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara.