Waziri mwakyembe amjulia hali rais wa zamani wa ZFA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, March 18, 2018

Waziri mwakyembe amjulia hali rais wa zamani wa ZFA

HABARI KUU

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amemjulia hali Rais wa zamani wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Ali Ferej Tamim nyumbani kwake Shangani Mjini Unguja ambae anasumbuliwa na Uti wa Mgongo.
Mwakyembe ambaye ameongozana na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo, Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said.
Mwakyembe amesema ameona haya ya kumtembelea mwana michezo huyo kutokana na kazi kubwa aloifanya katika taifa la Tanzania.
Nae Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) amesema kutokana na kuongoza vyema ZFA pamoja na kuitangaza Zanzibar kimataifa wameona haja ya kumtembelea.
Kwa upande wake Rais wa zamani wa ZFA Ali Ferej Tamim amewashukuru na kuwapongeza viongozi hao kwenda kumjulia hali huku akisema kwasasa amepata afadhali na kuendelea kufata ushauri wa Daktari.
Mapema leo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Ali Karume kwa lengo la kujuwana na kupanga mikakati yao ikiwemo masuala ya michezo yanayogusa pande zote mbili za Muungano wa Tanzania.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI