Taasisi ya Samael kushirikina na Serikali Mkoa wa Kusini Pemba - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, March 29, 2018

Taasisi ya Samael kushirikina na Serikali Mkoa wa Kusini Pemba

HABARI KUU

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Abdalla Rashid Ali, akimkabidhi zawadi mtoto Yatima baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Samael Academy, Sheikh Nassir Bin Said Al-Rawahy, huko Gombani Pemba.

Mkurugenzi wa taasisi ya Samael Academy, Sheikh , Nassir Bin Said Al-Rawahy, akibadilishana mawazo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Chake Chake  Abdalla Rashid Ali, katika hafla ya utowaji wa Zawadi kwa watoto Mayatima , ilioandaliwa na taasisi hiyo.

PICHA NA OMAR MJAKA  KUTOKA TAASISI YA SAMAEL ACADEMY.



Na Aziz Simai, Pemba

Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba, imeahidi kushirikiana na taasisi ya Samael Academy iliyoko Gombani Chake-Chake Pemba, ili iweze kufikia malengo ya kutoa elimu bora kwa jamii.

Akizungumza katika hafla fupi ya utoaji sadaka kwa watoto yatima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Katibu Tawala Wilaya ya Chake-Chake Pemba, Abdalla Rashid Ali, alisema  malengo ya taasisi hiyo ni faraja kwa Mkoa huo katika utoaji wa elimu ya fani mbali mbali ikiwemo elimu ya ufundi kwa vijana.

Katibu Tawala  huyo ,alieleza  kuwa Serikali ya Mkoa huo pamoja na Wilaya zitajitahidi kushirikiana ili kuona changamoto zilizoikabili Taasisi hiyo yaSamael academy inapatiwa ufumbuvi wa haraka ili shughuli za Taasisi ziweze kuanza mara moja.

Akizungumza malengo makuu ya Taasisi hiyo , Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Samael academy, Sheikh  Nassir Said Al-Rawahy alisema wamekusudia kufundisha   masomo mbali mbali yakiwemo ya biashara na ufundi lakini shuhuli hizo zimechelewa kuanza   kutokana na kuchelewa kupata usajili kutoka baraza la mitihani Tanzania (NACTE).

Sheikh Nassir, alifahamisha  mbali na hilo  Taasisi hiyo inaendelea na shughuli zake nyengine ikiwemo ujenzi wa miskiti, uchimbaji wa visima, kutoa sadaka kwa mayatima na kusaidia shughuli za madrasa za Qur-an.

Katika hafla hiyo jumla ya wanafunzi  100 mayatima, walipatiwa sadaka ya fedha taslim pamoja na zawadi nyengine mbali mbali.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI