HABARI KUU
Kabka ya mechi ya jana kati ya Watford na Chelsea mchezaji wa
zamani wa Manchester United Wayne Rooney aligeuka mchambuzi katika
kituo maarufu cha michezo nchini UK cha Sky Sports.
Moja kati ya mambo makubwa ambayo Wayne Rooney aliyazungumzia ni
kuhusu wachezaji watatu ambao wamekuwa katika vichwa vya habari vingi
katika siku za usoni (Paul Pogba, Henrikh Mkhitaryan na Alexis Sanchez).
Kwanza kuhusu Henrikh Mkhitaryan na Alexis Sanchez, kuhusu
Mkhitaryan, Rooney anaamini mchezaji huyo kwa sasa yuko katika sehemu
sahihi zaidi tofauti na alipokuwa katika klabu ya Manchester United.
Wayne Rooney ambaye alikuwa pamoja na Mkhitaryan katika kikosi cha
United na anasema Mualmernia huyo ana kipaji kikubwa sana lakini
alishindwa kuwa bora kutokana na kukosa uhuru aliokua akiupata United.
Kuhusu Sanchez, Rooney anaamini bila shaka kwamba Sanchez ni mtu
sahihi kabisa kwa Manchester United na hata ukimuangalia tu jinsi
ameingia katika klabu hiyo anaonesha amekuja kikazi zaidi.
Rooney anasema kati ya vitu Romelu Lukaku alivyokuwa anavikosa ndani
ya Manchester United ni wachezaji ambao wanamsukuma mbele ili afunge na
ujio wa Sancheza unaweza kuwa tiba la suala hilo.
Paul Pogba, Wayne anasema kama Pogba akipunguziwa majukumu anaweza
kuwa bora zaidi kwani Pogba ni mzuri zaidi akicheza box to box midfilder
na kwa uwepo wa Matic inaweza kumuimarisha siku hadi siku.
Kuhusu Manchester City Rooney ameweka wazi kwamba kuwakamata
haiwezekani na akasisitiza kwamba kwa jinsi wanavyocheza soka hata msimu
ujao pia inawezekana wasikamatike.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Tuesday, February 06, 2018
Rooney avunja ukimya kuhusu Sanchez, Mkhitaryan, Paul Pogba na Man City
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.