NAHODHA NA BEKI TEGEMEO AZAM FC, AGGREY MORRIS ASEMA SIMBA WATAKOMA KESHO - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, February 06, 2018

NAHODHA NA BEKI TEGEMEO AZAM FC, AGGREY MORRIS ASEMA SIMBA WATAKOMA KESHO

HABARI KUU

 NAHODHA Msaidizi Azanm FC, Aggrey Morris Ambroce amesema kwamba hawataangusha mashabiki wao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza Saa 10.00 jioni, unatarajia kuwa mkali ya wa aina yake kutokana na Azam FC iliyojikusanyia pointi 33 kuwa kwenye vita kali ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi, walio kileleni kwa pointi zao 38.
Beki wa kati, Morris amewataka mashabiki kuondoa hofu na kuwaomba kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti.


Aggrey Morris amesema kwamba hawatawaangusha mashabiki wao katika mchezo dhidi ya Simba kesho 

“Kwanza tunamshukuru Mungu wachezaji wako katika morali ya hali ya juu yaani inaonyesha wachezaji kila mmoja anajiandaa kuhakikisha kutaka kushinda mchezo huu,” alisema.
Moris alikiri ushindani utakuwa mkubwa kutokana na Simba kuwa kileleni mwa ligi, na kudai kwa sasa timu yake imeongezewa morali kutokana na ushindi wa juzi walipoichapa Ndanda mabao 3-1.
“Hiyo inatupa morali zaidi ya kwenda kupambana kwa sababu sisi lengo letu ni kushinda mchezo huu kujihakikishia tunaifukuzia Simba katika nafasi ya juu,” alisema.
Tayari kikosi cha Azam FC kinachodhaminiwa na Benki ya NMB, Maji Safi ya Uhai Drinking Water na Tradegents, kimeshaanza maandalizi jana jioni kuelekea mchezo huo na wachezaji wakiendelea kukaa kambini tokea ulipomalizika mtanange dhidi ya Ndanda, yote hiyo ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha inaibuka na pointi zote tatu.
Aidha itakumbukwa kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex Septemba mwaka jana, timu hizo zilitoka suluhu.
Ushindi wowote wa Azam FC kwenye mchezo huo, utazidi kupunguza pengo la pointi baina yake na Simba na kufikia mbili na hivyo kuendeleza mapambano ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo, walioutwaa mara ya mwisho msimu wa 2013/2014.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI