CAF waiwashia Cameroon “taa ya kijani” maandalizi ya AFCON 2019 - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, February 06, 2018

CAF waiwashia Cameroon “taa ya kijani” maandalizi ya AFCON 2019

HABARI KUU
Kulikuwa na mashaka juu ya uandaaji wa michuano ya AFCON mwaka 2019 ambapo nchi ya Cameroon ndio wanatari kuwa wenyeji wa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza June 7 hadi July 7 mwakani.

Kulikuwa na taarifa na hofu kwamba Cameroon hawako tayari kimiundombinu pamoja na kiuchumi kuandaa michuano hiyo mikubwa Afrika na ilibidi CAF kuanza kuchunguza maandali ya michuano hiyo.

Baada ya uchunguzi huo CAF wametoa ruhusu kwa Cameroon kuendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo baada ya timu ya maafisa wa CAF kuridhishwa na maandalizi yanayoendelea nchini humo.

Juniour Binyam mwenyekiti wa kamati ya masuala ya habari wa CAF amethibitisha hilo na kusema kwamba CAF kwa sasa hawana mashaka juu ya maandalizi ya michuano hiyo na wanaona hadi kufika wakati huo Cameroon watakuwa tayari.
 
Inatajwa moja ya sababu kubwa iliyokuwa inatoa mashaka kwa CAF kutowaamini sana Cameroon ni kutokana na ongezeko la timu kutoka 16 kwenda hadi 24 jambo ambalo ilidhaniwa inaweza kuwasumbua Cameroon lakini wanaonekana wanaweza kukabiliana nalo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI