MAPEMAA, AL MASRY NAO WATUMA MTU KWENDA KUIFANYIA UPELELEZI SIMBA IKICHEZA DJIBOUTI - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, February 18, 2018

MAPEMAA, AL MASRY NAO WATUMA MTU KWENDA KUIFANYIA UPELELEZI SIMBA IKICHEZA DJIBOUTI

HABARI KUU



Wakati Simba imetuma mtu mapema kwenda Djibouti kwa ajili ya maandalizi ya mechi ijayo dhidi ya Gendamarie, wanaotarajiwa kuwa wapinzani wao wameonyesha nao wako makini zaidi.
Al Masry ya Misri wanajipa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika Kombe la Shirikisho dhidi ya Buffaloes ya Zambia baada ya kushinda kwa mabao 4-0 mechi ya kwanza.
Kutokana na hivyo, wametuma mmoja wa watu wa ufundi kutoka katika benchi lao kuangalia uchezaji wa Simba, hasa inapokuwa ugenini.
“Tayari kuna mtu ameandaliwa kwenda Djibouti kuangalia mechi ya mwisho ya Simba. Hata kama itakuwa nyepesi lakini watapata uhakika namna ya mchezo wao.
“Wanafanya mambo mawili kwa wakati mmoja, hapo wanajiandaa na mechi ya pili huko Zambia. Wana asilimia themanini ya kuvuka. Hapo hapo wameanza kujiandaa na Simba,” alisema Mtanzania anayeishi nchini baada ya kuzungumza na SALEHJEMBE.

Iwapo Simba itavuka, basi ina nafasi kubwa ya kukutana na Al Masry ambayo inaonekana Simba watalazimika kufanya maandalizi ya uhakika hasa.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI