Kenya yafuzu AFCON 2019 baada ya miaka 15, Sierra Leone yaondolewa - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


nuru+ya+habar

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Tuesday, December 04, 2018

demo-image

Kenya yafuzu AFCON 2019 baada ya miaka 15, Sierra Leone yaondolewa

Responsive Ads Here

ARATimu ya taifa ya soka Kenya, Harambee Stars, imefuzu katika fainali ya mataifa bingwa mwaka 2019.
Hatua hii imekuja, baada ya uamuzi wa kamati kuu ya CAF, kuamua kuiondoa Sierra Leone katika michuano ya kufuzu,baada ya kufungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Hii inaamanisha kuwa Kenya ambayo ipo katika kundi F, pamoja na Ghana na Ethiopia, itakuwa miongoni mwa timu mbili zitakazofuzu, hata iwapo itashindwa katika mechi yake ya mwisho ya kundi hilo mwezi Machi mwaka 2019.

Harambee Stars inaongoza kundi hilo kwa alama saba, mbele ya Ghana ambayo ina sita. Mara ya mwisho kwa Kenya kucheza katika fainali ya kombe la Afrika likuwa ni miaka 15 iliyopita, nchini Tunisia.

Post Bottom Ad

HABARI

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *