Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko katika jeshi hilo na kuwabadili baadhi ya makamanda vyeo vyao vya kazi akiwemo RPC wa Mtwara Lucas Mkondya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, aliyekuwa Kamanda wa Polisi jijini Mwanza, Ahmed Msangi ambaye sasa amekuwa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya Msemaji wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa, ambapo amesema kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida.
“Aliyekuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Barnabas Mwakalukwa, anakwenda kuwa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Pwani huku aliyekuwa mnadhimu wa Pwani sasa anakwenda kuwa RPC wa mkoa wa Mtwara akichukua nafasi ya Lucas Mkondya aliyehamishiwa kitengo cha Intelijensia ya Makosa ya Jinai Makao Makuu Dar es salaam,”amesema Sirro
Hata hivyo, katika hatua nyingine, Kamanda Msangi amewatahadharisha waganga wa kienyeji wanaotumia ramli chonganishi kuacha mara moja kwa kua tayari makamanda wote wa jeshi hilo hapa nchini wameshapewa maelekezo kuhusiana na watu hao ambao wanakwenda kinyume cha sheria na taratibu.