Mahakama nchini Tanzania yawahukumu wachina watatu Jela - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, November 09, 2018

Mahakama nchini Tanzania yawahukumu wachina watatu Jela

HABARI KUU 
Washtakiwa hao ni Injinia Xia Yanan (26), Chen Jinchuan (31) na Mtala Habibu (29) fundi umeme.Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Nassoro Katuga kuwasomea washtakiwa makosa yao na kukiri.
Hakimu Shaidi amesema kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao anawahukumu kulipa faini ya Shilingi Milioni Tisa na Laki Tatu ama kwenda jela miaka 2 kwa washtakiwa wote.
Washtakiwa hao wamefanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka wanadaiwa kati ya January na August 28,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni ambapo waliendeleza ujenzi bila kuchukua tahadhari ya mazingira kutoka NEMC.
Pia wanadaiwa kutenda kosa la kutotii amri (NEMC) August 25,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni Dar es Salaam, ambapo walishindwa kutii amri halali kupitia barua ya NEMC ya kusimamisha ujenzi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI