KUHUSU AZAM FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA, UONGOZI WAFUNGUKA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, November 21, 2018

KUHUSU AZAM FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA, UONGOZI WAFUNGUKA

HABARI KUU
Uongozi wa timu ya Azam FC, umesema kuwa hatma ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima na Kiungo mkabaji wa Yanga Papy Tshishimbi upo mikononi mwa kocha mkuu Hans Pluijm.

Niyonzima na Tshishimbi wamekuwa wakihusishwa kujiunga na Azam FC kwenye dirisha dogo lilifunguliwa Novemba 15 huku Azam wakiwa wameshamsajili Obrey Chirwa kwa kandarasi ya mwaka mmoja.


Ofisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema kuwa suala la wao kufanya usajili hilo lipo wazi ni lazima waboreshe kikosi chao kutokana na ushindani uliopo.


"Pluijm ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya wachezaji hao, tunatambua kwamba wana mikataba na timu zao, tutafanya kazi kwa kuzingatia utaratibu kama kutakuwa na uhitaji wa kuwasajili tutafanya hivyo.


"Kwa sasa hatuna mazungumzo nao kwa kocha hajasema kama anawahitaji tunaangalia namna ya kuweza kuwa bora zaidi ya msimu uliopita," alisema.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI