DEMBELE, GOMES, FABREGAS, HAZARD, RICE, ALBA: TETESI KUBWA NA KALI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, November 26, 2018

DEMBELE, GOMES, FABREGAS, HAZARD, RICE, ALBA: TETESI KUBWA NA KALI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO

HABARI KUU

Mfaransa Ousmane Dembele, 21, ameomba kuondoka Barcelona mwezi Januari na kuondoka kwake kutamruhusu Neymar kurudi Nou Camp kutoka Paris St-Germain. (Goal)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27 amekana kuwa atahamia Paris St-Germain, lakini amekiri kuwa ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (Canal+ via Goal)

Mkurugenzi wa Milan Leonardo ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31, na walinzi Gary Cahill, 32, na Andreas Christensen, 22. (Football Italia)

Manchester United ilituma maajenti kumtazama kijana mlinzi wa West Ham Declan Rice, 19, wakati Hammers walishindwa kwa mabao 4-0 na Manchester City siku ya Jumamosi. (Metro)

Beki wa Barcelona Jordi Alba, 29, amekiri kuwa hajapewa mkataba mpya klabuni na kuacha hatma yake gizani. (ESPN)

Manchester United wanaweza kungoja kumsaini kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini baada ya kugundua kuwa kupengee cha kuuvunja mkataba wake kinaweza kutumiwa mwisho wa msimu. (Mirror via Manchester Evening News)

Meneja wa Newcastle Rafa Benitez anasema hataki kurejea kwa Serie A siku za usoni ikiwa ndoto yake haitatimia huko St James' Park. (Newcastle Chronicle)

Mlinzi wa Chelsea David Luiz alifichua kuwa Maurizio Sarri amekuwa mwenye hasira zaidi wakati wa ushindi kuliko wakati wa kushindwa kwao na Tottenham. (Mirror)

Pep Guardiola anasema shinikizo kutoka kwa mahasimu Liverpool inaweka kikosi chake cha Manchester City na motisha katika ulinzi wake katika Premier League. (Standard)

Kiungo wa kati wa Everton Seamus Coleman, 30, ametaja rekodi yake dhidi ya Liverpool kama ya kutia aibu. (Express)

Mshambulizi wa Santos Gabriel Barbosa, 22, anaweza kuwa tayari kwa jukumu moja huko Toffees baada ya kipindi kigumu huko Inter Milan. (Tutto Mercato Web - in Italian)

Mlinzi raia wa Sweden Mikae Lustig, 31, anatarajiwa kufanya mazungumzo wiki mbili zinazokuja ikiwa ataamua kuendelea kuwepo huko Celtic. (Daily Record)

Nahodha wa Leicester Wes Morgan, 34, ameitisha mazungumzo na marefa kuhusu maamuzi yasiyo ya kuridhisha. (Leicester Mercury)

Kutoka BBC

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI