Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 06, 2018

Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki

HABARI KUU
Mganga mmoja wa asili nchini Nigeria amefariki baada ya mteja wake kujaribu iwapo ana nguvu za kuzuia risasi kuingia mwilini mwake kama alivyodai.
Chinaka Adoezuwe , 26, aliuawa baada ya kumuagiza mteja wake kumpiga risasi alipokuwa akivaa nguvu hizo za kuzuia risasi katika shingo yake.
Maafisa wa polisi katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo wanasema kuwa mteja huyo sasa amekamatwa kwa madai ya mauaji
Nguvu za uganga ni maarufu nchini Nigeria , ambapo waganga huombwa kuwatibu raia magonjwa tofauti.
Lakini kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kula nguvu za kuzuia risasi na dawa.
Kijana mmoja alikuwa amemtembelea mganga huyo ili kupata nguvu za kuzuia risasi ambazo mganga huyo alimpatia, kulingana na mwanakijiji mmoja aliezungumza na gazeti la Punch.
Ili kuthibitisha kwamba nguvu hizo zinafanya kazi , alisimama na kumpatia mteja wake bunduki. Na hapo ndipo janga likatokea!.
Mnamo mwezi Januari , muuzaji wa dawa za kienyeji alikamatwa baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kunywa maji ya kuzuia risasi kuuawa.
Muuzaji huyo anayeishi kaskazini magharibi mwa Nigeria aliripotiwa kumhakikishia mtu huyo kwamba hatofariki atakapopigwa risasi.
Chanzo-BBC

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI