Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) Yapunguza Asilimia ya Riba Kutoka 18% Hadi 12% Kwa Wateja Wake Wanaochukua Mkopo. - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, June 02, 2018

Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) Yapunguza Asilimia ya Riba Kutoka 18% Hadi 12% Kwa Wateja Wake Wanaochukua Mkopo.

HABARI KUU
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) Ndg. Juma Amour Khafidh akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusia na benki yake kupungua riba kwa wateja wake wanaochukua mikopo kwa kiasi kikubwa na kusema Wananchi na Wateja wa PBZ watanufaika na punguzo hilo na kutowa fursa Wananchi na Wafanyakazi wa Serikali kufaidika ba punguzi hili na kujikomboa na umasikini kwa kuweza kuwekeza katika maisha ya baadae.Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Jengo la Bima Mpirani Zanzibar.  
Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali wakifuatilia taarifa hiyo kwa makini wakati wa mkutano wao na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Amour Khafidh uliofanyika katika majengo ya Bima mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Amour Khafidh akitowa ufafanuzi kuhusiana na punguzo hilo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano wake na kusema PBZ kwa mwaka wa fedha imepiga hatua na kuongeza kwa faida kwa kiasi kikubwa.   
Maofisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) wakifuatilia taarifa hiyo wakati ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Amour Khafidh katika ukumbi wa mkutano wa Makao Makuu uliopo katika majengo ya Shirika la Bima Mpirani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Amour Khafidh akifuatilia maswali akiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika makao makuu ya PBZ mpirani Zanznzibar kulia Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi. Khadija Shamte Mzee.
Mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Ndg. Farouk Karim akiuliza swali kuhusiana na hatua hiyo ya PBZ kushusha riba kwa wateja wake wanapochukua mikopo kupitia PBZ.
Mwandishi wa Habari muandamizi Zanzibar Ndg. Issa Yussuf akiuliza suali kuhusiana na mikopo kichefuchefu wakati wa mkutano huo na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Amour Khafidh, wakati wa mkutano huo wa kutowa mafanikio ya Benki ya Watu wa Zanzibar limited kwa mwaka huu.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI