JERRY MURO AWAOMBA WANAYANGA WAACHE KUPIGA KELELE, WAICHANGIE TIMU - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, May 09, 2018

JERRY MURO AWAOMBA WANAYANGA WAACHE KUPIGA KELELE, WAICHANGIE TIMU

HABARI KUU

Na George Mganga


Afisa Habari wa zamani katika klabu ya Yanga, Jerry Muro, amewaomba wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuichangia fedha badala ya kupiga kelele mitandaoni.

Yanga imekuwa na hali ambayo si rafiki kifedha ambapo inaelezwa kuwa ina madeni kwa baadhi ya wachezaji wake tofauti na miaka kadhaa iliyopita wakati ikifadhiliwa na Mfanyabiashara, Yusuph Manji.

Muro amewaomba Wanayanga wote kutumia muda wao kuichangia ili wachezaji wake waweze kupata morali na motisha ya kuipigania timu.

Kiongozi huyo aliyechukuliwa nafasi yake na Dismas Ten, anaamini kama mashabiki wa klabu hiyo kongwe wataweza kuichangia, yawezekana tatizo la fedha likawa na ahueni kutokana na inavyopitia wakati mgumu kwa sasa.

Muro ameeleza kuwa baadhi ya mashabiki wamekuwa wakilalamika kuhusiana na mwenendo wa Yanga ulivyo hivi sasa huku wakisahau kuwa inawategemea wao wanachama kwa ajili ya kuipa nguvu ikiwemo kuichangia.

Taarifa zinaelezwa kuwa Yanga inahaha kulipa mishahara ya wachezaji wake kwa sasa na hata kuondoka kwa Kocha George Lwandamina inaelezwa ni madai ya fedha za mshahara wake kutolipwa.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI