Imeandikwa na mwandishi wetu.
Katibu tawala wilaya ya wete Mkufu Faki Ali amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari kwa kuweka mazingira safi na kujikinga na maradhi ya miripuko .
Kauli hiyo ameitowa wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa ya wilaya hapo ofisini kwake wete mkoa wa kaskazini pemba.
Amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ni vyema wananchi kuchukuwa tahadhari za maksudi kusafisha maeneo yao pamoja na kuondoa miti hatarishi iliokaribu na makaazi ambayo inaweza kusababisha maafa.
Aidha amesema kumekuwa na baadhi ya wananchi hujenga kwa maksudi katika maeneo hatarishi kwa lengo la kuona kwamba serekali itatoa misaada kwa waathirika wa maafa hayo.
Wakichangia katika kikao hicho wajumbe wa kamati hiyo ya maafa wamesema ni vyema kutolewa elimu kwa wananchi juu ya uwekaji wa mazingira safi katika kipindi hichi cha mvua ikiwemo kuchemcha maji kabla ya kunywa kuweka dawa za water gurd kusafisha mitaro ya maji machafu pamoja na kunawa kwa sabuni wanapotoka chooni.