WATU 200 WAZAWADIWA TIKETI ZA TAMASHA LA KIMATAIFA LA TUZO ZA FILAMU - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, March 29, 2018

WATU 200 WAZAWADIWA TIKETI ZA TAMASHA LA KIMATAIFA LA TUZO ZA FILAMU

HABARI KUU

200 wapata tiketi za bure kuingia kwenye usiku wa tuzo,
Aprili Mosi 2018.


Wakazi zaidi ya 200 wa jiji la Dar es Salaam wamepata fursa ya kuingia bure kwenye Tamasha la Kimataifa la Tuzo za Filamu la Sinema Zetu (SZIFF), litakalofanyika Jumapili, Aprili Mosi mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.


Wadau hao wamepata fursa hiyo kupitia zoezi la ugawaji wa tiketi hizo mitaani kwa njia ya kuuliza maswali na washindi kupata tiketi za bure, likiongozwa na wasanii wa filamu,
Hashim Kambi pamoja na Yvonne Cherrie (Monalisa), chini ya Kampuni ya Azam TV ambao niyo waandaji wa tamasha hilo.

Zoezi hilo limefanyika kwa siku mbili mfululizo (Machi 27 na 28, mwaka huu) katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yakiwakilishwa na vituo vinane ambavyo ni
Tabata Segerea, Gongo la Mboto, Tandika, Mbagala, Ubungo, Kimara, Tegeta na Kawe.







Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI