Maguli kazungumza kuhusu kurudi uwanjani baada ya kukaa nje miezi 6 - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, March 29, 2018

Maguli kazungumza kuhusu kurudi uwanjani baada ya kukaa nje miezi 6

HABARI KUU
Mshambuliaji wa zamani wa Ruvu Shooting, Simba, Stand United za ligi kuu tanzania bara na Dhofar ya Oman Elias Maguli baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi sita bila kucheza, hivi karibuni atatangaza timu atakayocheza msimu ujao.
Maguli ambaye walishindwa kufikia mwafaka na Polokwane City ya Afrika kusini iliyokuwa ikitaka kumsajili kipindi cha dirisha dogo alichelewa usajili wa tanzania hivyo kulazimika kukaa nje kwa kukosa timu.
Mshambuliaji huyo amesema siku si nyingi atatangaza timu atakayocheza msimu ujao, inawezekana ikawa ya VPL au nje ya nchi.
“Sasa hivi watu wanapambana kuzinusuru timu zao zisishuke daraja wengine wanataka ubingwa kwa hiyo wapo makini sana na ligi kumalizia mechi zilizobaki, watakapomaliza michakato ya usajili itaanza kwa hiyo nitajua ni hapa nyumbani au nje.”
“Msimu ujao au hivi karibuni naweza nikaweka wazi ni wapi nitaelekea kwa sababu ndani ya miezi sita nimekaa bila kucheza.”

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI