Houston: Mwanaume aliyetembea na suruali yake miguuni auawa na polisi Marekani - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, March 29, 2018

Houston: Mwanaume aliyetembea na suruali yake miguuni auawa na polisi Marekani

HABARI KUUDanny Ray ThomasKulingana na ndugu zake mkewe Bw. Thomas aliwauwa watoto wake wawili mwaka 2016Afisa wa polisi nchini Marekani amempiga risasi na kumuua mtu ambaye hakuwa na silaha aliyekuwa akitembea barabarani huku suruali yake ikiwa miguuni.
Familia yake inasema mauaji hayo yanaonekana yaliyokuwa ''yamepangwa''
Kamera za video ya polisi inaonyesha kuwa Danny Ray Thomas, mwenye umri wa miaka 34, akitembea mkabala na afisa wa polisi kwenye barabara mjini Houston, Texas, Alhamisi iliyopita kabla ya kumpiga risasi.
Afisa huyo wa polisi Cameron Brewer alirudia mara kadhaa akipaza sauti "lala chini ardhini" kabla ya kufyatua risasi.
Polisi na mwathiriwa wote ni Wamarekani weusi.
Familia na Thomas inasema kuwa alikuwa na tatizo la msongo wa mawazo tangu alipofiwa na mtoto wake.
Dada yake, Kita Thomas-Smith, alihudhuria mkutano wa baraza la jiji la Houston Jumanne ambako aliwataka wanasiasa kuchukua hatua juu ya "ukatili wa polisi".
Meya Sylvester Turner alimwambia kuwa: "kusema ukweli ninahisi maumivu yako. Tunaomba msamaha kwa maisha yoyote yaliyopotezwa."
Nje ya ukumbi wa jiji, Bi Thomas-Smith alikieleza kitengo cha kamera za video za barabarani cha Houston kwamba . "anahisi kama mauaji hayo yalipangwa.
" Ni wazi hakuwa anakimbia, kuwa alikuwa anatembea, kuelekea alikokuwa afisa wala hakuwa akijaribu kumuumiza ."

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI