Baada ya kutolewa “Hatuwezi kutumia uwanja wa nyumbani”-Cannavaro - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, March 18, 2018

Baada ya kutolewa “Hatuwezi kutumia uwanja wa nyumbani”-Cannavaro

HABARI KUU
Baada ya Yanga kushindwa kufuzu kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa kutolewa na Township Rollers ya Botswana, nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amejata sababu ya kuondolewa katika mashindano hayo.
Cannavaro amesema sababu kubwa ya kushindwa kusonga mbele ni kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani.
“Kitu ambacho kimetufanya tusisonge mbele ni kwamba, hatuwezi kutumia uwanja wa nyumbani, kama tungeweza kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani tungefuzu lakini kitu ambacho kimetuangusha ni kufungwa 2-1 nyumbani na mashindano haya lazima ushinde nyumbani ili ufuzu.”
“Ugenini kuna mambo mengi sana kama hujashinda nyumbani unapata matatizo mengi. Tunamshukuru Mungu tumemaliza salama sasa tutajiandaa na kombe la shirikisho.”
“Nawaomba wanayanga na watanzania kwa ujumla tuweze kucheza viwanja vya nyumbani, ugenini kuna mambo mengi yanatokea lakini kwa sasa tuelekeze kila kitu kwenye mechi za kombe la shirikisho ili tuweze kufanya vizuri kwa sababu bado tupo kwenye mashindano.”

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI