Wakaazi Elfu 16 Kondoa Vijijini Waondokana na Kero ya Maji. - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, February 02, 2018

Wakaazi Elfu 16 Kondoa Vijijini Waondokana na Kero ya Maji.

 
 
HABARI KUU

Na Benny Mwaipaja, Kondoa
ZAIDI ya wakazi elfu 16 wa vijiji vitatu vya Mauno, Makiranya na Kinyasi-Majengo, katika Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma wameondokana na adha ya kukosa maji baada ya kuzinduliwa kwa visima viatu vya maji vilivyojengwa kwa msaada wa wahisani kutoka nchini Uturuki kupitia ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa visima hivyo katika Kijiji cha Mauno, Kata ya Bumbuta, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini Dokta Ashatu Kijaji, amesema kuwa kuzinduliwa kwa visima hivyo kunalifanya jimbo lake lifikishe visima 41 hatua ambayo amesema itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika jimbo lake.

Dkt. Kijaji ameushukuru Ubalozi wa Uturuki kwa kuratibu msaada huo wa zaidi ya Dola za Kimarekani elfu 36, sawa na shilingi milioni 81, zilizotumika kuchimba visima hivyo pamoja na kuweka miundombinu mingine zikiwemo jenereta zinazotumika kusukuma maji hayo na kuwezesha upatikanaji wa maji hayo.

"Hivi sasa ujenzi wa visima 15 kati ya 25 vinavyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji unaendelea huku wahisani wakiwa wametujengea visima 36 hivyo kufikisha idadi ya visima 61 katika kipindi cha miaka miwili tu tangu Serikali ya Awamu ya Tano ya  Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aingie madarakani hali ambayo haijawahi kutokea na lengo letu ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote 84 vinapatiwa huduma ya maji ifikapo mwaka 2020" Alisisitiza Dkt. Kijaji

Diwani wa Kata ya Bunbuta Bw. Bashiru Mtolo na mkazi mmoja wa kijiji hicho Bi. Khadija Hussein wamesema kuwa tatizo la maji katika kijiji cha Mauno lilikuwa kubwa na kuwalazimisha wanawake na watoto kwenda umbali mrefu kusaka maji kwa ajili ya matumizi yao ya majumbani pamoja na kunywesha mifugo.

"Tunaushukuru Ubalozi wa Uturuki kwa msaada wao huu mkubwa na Mbunge wetu kwa ufuatiliaji wake wa karibu uliowezesha kupatikana kwa visima hivi na vingine ambavyo vimesaidia kwa kiwango kikubwa kutatua kero ya maji na tunaamini mpaka kufikia mwaka 2020, matatizo ya maji katika wilaya yetu ya Kondoa litakuwa historia" alisema Diwani Mtolo.

Naye Mwakilishi na Mwambata wa Ubalozi wa Uturuki hapa nchini Sheikh Muhammad Cicek ameeleza kuwa msaada wa Dola elfu 36 zilizotumika kujenga miradi hiyo mitatu ya visima vya maji umetolewa na wahisani mbalimbali wa Uturuki ikiwa ni kuenzi uhusiano wa muda mrefu kati ya Uturuki na Tanzania.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo ya maji kutasadia kuwawezesha akina mama na wananchi wa Kondoa kwa ujumla kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji ambayo hata hivyo hayakuwa safi wala salama.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI