BAADA YA KUPOTEZA KWA YANGA, AZAM FC YAMALIZA HASIRA KOMBE LA SHIRIKISHO, YAPIGA MTU 5-0 - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, January 30, 2018

BAADA YA KUPOTEZA KWA YANGA, AZAM FC YAMALIZA HASIRA KOMBE LA SHIRIKISHO, YAPIGA MTU 5-0

HABARI KUU



Ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, Azam FC imeibukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kutoa adhabu kali.

Timu hiyo, ilivana na Shupavu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili katika mchezo huo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mechi hiyo shujaa wa mchezo huo ni kinda, Paul Peter wa Azam ambaye alipiga ‘hat trick’ katika mechi hiyo katika ushindi wa mabao 5-0.

Katika mchezo huo Azam ilionekana kumiliki mpira vyema katika vipindi vyote viwili huku bao la kwanza kwenye mchezo huo  likifungwa dk 45 ya mchezo huku la pili likafungwa dakika hiyohiyo baada ya kuongezwa dakika mbili.

Peter alifunga mabao katika kipindi cha pili cha mchezo huo akifunga dakika ya 57, 77  na 88 huku timu yake ikitangulia katika hatua hiyo ya 16 bora.


Mabao mengi ya timu hiyo yalifungwa na Yahya Zaydi katika dakika ya 45 kwa njia ya penalti kabla ya Iddi Kipagulile kumchabua kipa wa Shupavu katika dakika za nyingeza baada ya kuwatoka mabeki wa timu hiyo.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI