LIVE: YANGA 4-1 MAJIMAJI, FULL TIME, KIPINDI CHA PILI, UWANJA WA TAIFA, LIGI KUU BARA - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, February 14, 2018

LIVE: YANGA 4-1 MAJIMAJI, FULL TIME, KIPINDI CHA PILI, UWANJA WA TAIFA, LIGI KUU BARA

HABARI KUU


FULL TIME

Kipindi cha pili kimekamilika. Yanga inapata ushindi wa mabao 4-1.

Dk ya 90 + 1: Nahodha wa Majimaji, Hamis anapewa kadi ya njano.

Dk ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dk ya 88: Majimaji wamekata tamaa, kasi yao imepungua.

Dk ya 85: Yanga wanamtoa Dante anaingia, Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Tshishimbi anaipatia Yanga bao la nne kwa shuti kali kutoka nje ya 18.

Dk ya 81: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 81: Majimaji wanakosa nafasi ya wazi, mpira unapita pembeni kidogo ya lango.

Dk ya 79: Yanga wanapata faulo nje ya eneola 18, anapiga Chirwa, mpira uantoka nje.

Dk ya 76: Majimaji wanapata kona.

Dk ya 72: Mapunda anapiga kona, mpira unaokolewa.

Dk ya 71: Majimaji wanafanya shambulizi, inakuwa kona.

Dk ya 70: Hassan Kessy anapewa kadi ya njano kwa Yanga.

Dk ya 67: Yanga wanafanya shambulizi lakini mpira unatoka nje. 

Dk ya 61: Majimaji wamepata uhai, wanapiga pasi na kushambulia.

Dk ya 56:  Marcel anapiga na kufunga.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 55: Juma Said 'Makapu' anaunawa mpira ndani ya eneo la 18, inakuwa penalti.

Dk ya 52: Chirwa anakosa nafasi ya wazi akiwa karibu na lango la Majimaji.

Dk ya 51: Majimaji wanabadilisha wachezaji wawili kwa mpigo.

Dk ya 49: Majimaji wanafika langoni mwa Yanga.

Dk ya 48: Timu zinaanza kusomana.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Dakika ya 45 + 1: Mwamuzi anamaliza kipindi cha kwanza.

Dk ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika moja ya nyongeza.

Emmanuel Martine anapiga mkwaju mkali unajaa wavuni. Ni moja ya mabao mazuri msimu huu.

Dk ya 43: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 42: Six wa Majimaji anapiga shuti linatoka nje ya lango la Yanga.

Dk ya 39: Buswita anapiga mkwaju unagonga nguzo.

Dk ya 37: Yanga wanamiliki mpira.

Dk ya 35: Majimaji wamepunguza kasi.

Dk ya 30: Refa anampa kadi ya njano Chirwa kwa kuvua jezi yake licha ya kwua hakuitoa mwilini kabisa.

Yanga wanapata bao la pili, Obrey Chirwa anamalizia vizuri krosi ya Gadiel Michael kwa kichwa.

Dk ya 29: Gooooooooooooooooooooooo

Dk ya 27: Mchezo umekuwa mkali, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dk ya 21: Majimaji wanapangana.

Mchezaji mmoja wa Majimaji anapewa kadi nyekundu.

Papy Tshishimbi anaenda kupiga penalti, anafunga.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Mpoki Mwakinyuke anapewa kadi nyekundu kwa kuunawa mpira kwa makusudi na kusababisha penalti.

Mchezaji wa Majimaji anapata kadi nyekundu

Dk ya 17; Yanga wanapata penalti, Chirwa anaiwezesha Yanga kupata penalti.

Dk ya 10: Mchezo umeanza kuwa na kasi. Yanga wanatawala muda mwingi.

Dk ya 6: Majimaji wanajipanga.

Dk ya 2: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.

Yanga dhidi ya Majimaji, kumbuka katika mchezo wa kwanza wa timu hizi, zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.

Mchezo umenza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI