KUNA NJAMA ZA KUMUUMIZA JOHN BOCCO? MKUDE HUYU HAPA... - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, February 21, 2018

KUNA NJAMA ZA KUMUUMIZA JOHN BOCCO? MKUDE HUYU HAPA...




Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ameutaka uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuongeza umakini katika hatua ya lala salama ya Ligi Kuu Bara ili kuepukana na vitendo vya hujuma ambavyo vinajitokeza.

Mkude ametamka hayo baada ya kudai kuwa kuna njama ambazo zinafanyika na wapinzani wao katika ligi  kuwaumiza baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ili kuwapunguza kasi.

"Binafsi namkubali sana Bocco na anapokosekana katika kikosi chetu huwa sijisikii vizuri kwani ni mmoja kati ya washambuliaji wakuigwa hapa nchini."


“Ni mpambanaji na haogopi kuumia anapokuwa akipambana kuitafutia ushindi timu yetu, lakini kuna mchezo mchafu ambao umeanza kufanyika wa kutaka kumuumiza makusudi ili tu kuipunguza makali timu yetu, hiyo siyo sawa TFF wanatakiwa kuwa makini katika hilo,” alisema Mkude baada ya Bocco kuumizwa katika mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC.
HABARI KUU

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI