FIFA na CAF kuendelea kufikiria namna ya kuisaidia Zanzibar - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


nuru+ya+habar

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Sunday, February 25, 2018

demo-image

FIFA na CAF kuendelea kufikiria namna ya kuisaidia Zanzibar

Responsive Ads Here
HABARI KUU
PIX+1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad wakiri kuelewa hali ya Zanzibar pamoja na kuzingatia Sheria wamesema wanaona mazingira Maalum ya Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyozungumza na Marais hao wa mashirikisho ya mpira wa miguu kwa ngazi ya bara la Afrika na Dunia walipofika nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya mkutano wao wa kuandaa ajenda za mkutano mkuu wa dunia.

‘’Marais hao walisema kuondolewa kwa Zanzibar katika uanachama wa CAF kulizingatia sheria zinazosimamia Shirikisho hilo lakini pamoja na hayo waliamua kuiachia  Zanzibar kuendelea kufaidika na  fursa zote wanazopatiwa wanachama wa CAF  isipokuwa kuwaruhusu kupiga kura, pia wanasema wataangalia zaidi ya hilo maeneo mengine namna ya kuisaidia Zanzibar,''Dkt.Harrison Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika Mkutano huo Mheshimiwa Mwakyembe alisisitiza kuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alieleza kwa ufasaha mgogoro huu wa soka kwa viongozi hao wenyedhamana na mashirikisho hayo nao kumuelewa ambapo walisisitiza kuhitaji serikali kuendelea kushauriana nao katika suala hilo.


Pamoja na hayo nae Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia aliwasihi wapenzi wa soka nchini kuendelea kuwa watulivu kwani suala hilo linashughulikiwa na viongozi wa ngazi za juu nao wanalifahamu

Post Bottom Ad

HABARI

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *