BAADA YA KAULI YA HAJI MANARA, SALUM MKEMI NAYE AIBUKA NA KUTOA YAKE - NURU YA HABARI TZ

KWA HABARI ZA UHAKIKA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA


HABARI MPYA

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, February 09, 2018

BAADA YA KAULI YA HAJI MANARA, SALUM MKEMI NAYE AIBUKA NA KUTOA YAKE

HABARI KUU


Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kamwe hawana mpango wa kuishangilia Simba.

Kauli yake inakuwa ni kama kumjibu Msemaji wa Simba, Haji Manara ambaye aliomba Yanga isizomewe kesho pale Uwanja wa Taifa.

Mkemi amesema watakwenda Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia Simba wakivaana na St Louis ya Shelisheli, baada ya hapo, Jumapili Simba wataendelea na maisha yao.

“Sisi hatuna mpango wa kuishangilia Simba, hatuna kabisa. Mashabiki wa Yanga wakaishangilie timu yao.

“Hili suala la kuishangilia Simba kwetu halipo na halituhusu. Lakini nawaomba Wanayanga wajitokeze kwa wingi Jumamosi kuishangilia timu yetu,” alisema.

Siku chache zilizopita, Msemaji wa Simba, Haji Manara aliwaomba mashabiki na wanachama wa Simba kutoizomea Yanga Jumamosi kwa kuwa inacheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa mwakilishi wa Tanzania.


Kauli hiyo inaonyesha kuwakera baadhi ya mashabiki wako wakimpinga na wengine kumuunga mkono.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

HABARI