Mshambuliaji
wa Manchester City, Raheem Sterling (katikati) akinyoosha vidole juu
kushangili baada ya kuifungia timu yake bao la pili dakika ya 37 katika
ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Cardiff
City leo Uwanja wa Cardiff City katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la
FA England. Bao la kwanza lilifungwa na Kevin De Bruyne dakika ya nane
huku, Cardiff ikimpoteza mchezaji wake, Joe Bennett aliyetolewa kwa kadi
nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 90
HABARI KUU